User Registration

or Cancel
 • Maonesho ya Nanenane
  Maonesho ya Nanenane

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango akipata maelezo kuhusu shughuli za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini-GPSA  alipotembelea Banda la Wakala kwenye  Maonyesho ya siku ya Wakulima  Nanenane  iliyoadhimishwa Kitaifa  Mkoani Lindi mwaka 2017

 • Maonesho ya Nanenane
  Maonesho ya Nanenane

  Naibu Waziri wa Ardhi Dr.Angelina Mabula (MB) akiangalia bendera ya Taifa inayopatikana  katika ofisi za Wakala-GPSA  na kupata maelezo kuhusu shughuli zake  wakati alipotembelea banda la Wakala kwenye maadhimisho ya  siku ya Wakulima Nanenane Mkoani Lindi Kitaifa Mwaka 2017.

 • Mzabuni Akikabidhiwa Mkataba
  Mzabuni Akikabidhiwa Mkataba

  Kaimu Mkurugenzi wa Ununuzi na Ushauri Bi. Lilian Mwinuka akimkabidhi Mzabuni  mkataba maalumu wa vifaa na huduma mtambuka 2017/18, Bw. Edward Shayo ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kmpuni ya EA Brothers Contractors Company Limited.

 • PHOTOCOPY PAPER A4
  PHOTOCOPY PAPER A4

  MOJA YA BIDHAA ZA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI (GPSA) ILIYOINGIA KARIBUNI  NA INAPATIKANA KWA WINGI KWENYE MAGHALA YA WAKALA

 • UNUNUZI WA PAMOJA WA MAGARI
  UNUNUZI WA PAMOJA WA MAGARI

  HAYA NI BAADHI YA MAGARI YALIYONUNULIWA NA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI (GPSA) KUPITIA MFUMO WA UNUNUZI WA PAMOJA  KWA AJILI YA MAMLAKA YA HIFADHI ZA TAIFA  TANZANIA (TANAPA)

Chanzo: Tanzania Daima , 13 ,March 2014

WAKALA wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wakala za Serikali Na.  30 ya mwaka 1997, kupitia katika agizo la uanzishwaji wa Wakala.

Agizo la uanzishwaji lilifanyiwa mabadiliko kupitia tangazo Na. 133 la  Aprili 13, 2012 na kuzinduliwa Juni 16, 2008.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa GPSA, Josephat Mwambega, anasema jukumu la wakala huu ambao uko chini ya Wizara ya Fedha ni kununua, kuhifadhi na kusambaza vifaa vinavyohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya serikali.

Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 sura 410 na kanuni zake tangazo la Serikali Na. 446 la tarehe 20/12/2013.

Anasema jukumu hilo ndilo linalotumia rasilimali nyingi za wakala ikilinganishwa na majukumu mengine kwani ndilo jukumu linalopewa kipaumbele katika kupangia rasilimali muhimu kama fedha, watu na pia kupewa usimamizi makini.

Anasema jukumu hilo linatekelezwa katika mifumo miwili, kununua vifaa kwa ajili ya kutunza na kuuza, kuandaa utaratibu wa ununuzi wa pamoja wa vifaa na huduma mtambuka kwa kutumia mikataba maalumu.

Anasema kuanzishwa kwa wakala ni matokeo ya maboresho ya ununuzi katika sekta ya umma.

Serikali ilianza kufanya mabadiliko ya kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwa lengo la kuhakikisha umma unapata huduma bora.

“Sekta ya ununuzi kama zilivyo sekta nyingine ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yoyote ile.  Sekta hii ndiyo inayowezesha upatikanaji wa vifaa, mitambo, kazi za ujenzi, huduma za ushauri na zisizo za ushauri kutoka kwa wauzaji, watengenezaji, makandarasi, wataalamu wa ushauri na watoa huduma,” anasema Mwambega.

Anasema sekta hiyo ni kiungo muhimu kati ya muhitaji na muuzaji wa vifaa, kazi au huduma na ni mhimili mkubwa wa ukuzaji wa biashara ndani ya nchi na kati ya nchi moja na nyingine.

“Ununuzi huchangia katika upatikanaji wa ajira na uwezeshaji katika kutoa huduma za kijamii kama elimu, afya na maji.

“Takwimu zinaonesha kuwa ununuzi wa umma katika Tanzania unakadiriwa kutumia asilimia 70 hadi 80 ya bajeti ya serikali,” anasema na kuongeza kwamba kwa  kuzingatia umuhimu wa mchango wa ununuzi katika sekta ya umma.

Serikali ilianzisha Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini kwa malengo matatu ambayo ni kupunguza gharama za ununuzi katika sekta ya umma, kuongeza ufanisi wa Serikali kwa kuziwezesha taasisi kupata mahitaji yake ya vifaa na huduma zenye ubora n katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Ili kudhibiti udanganyifu katika utoaji wa mafuta kwa magari ya serikali, anasema wakala una mpango wa kufunga kifaa maalumu cha kidijitali kwenye kituo chake cha ugavi wa mafuta ya magari ya serikali, Kurasini, Dar es Salaam ili kuhakikisha hakuna upotevu wa mafuta unaotokea.

Majukumu mengine anasema ni kugomboa na kuondoa shehena bandarini na viwanja vya ndege, kutoa huduma ya kuhifadhi vifaa, kuandaa mikataba ya ununuzi wa vifaa na huduma zinazotumika mara kwa mara katika wizara, idara, wakala za serikali na taasisi za umma pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu katika nyanja za ununuzi na ugavi.

Mwambega anasema taasisi za umma kwa sasa zinabidi kuitekeleza Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 sura 410.

“Sheria hiyo inazitaka taasisi zote za umma kununua vifaa vya matumizi ya ofisini kutoka kwenye taasisi yake pekee. Inabidi wanunue vifaa hivyo kupitia kwetu kama hatuna kwa wakati huo inabidi tuwatafutie kwa wazabuni wetu kwa njia ya tenda,” anasema.

Anasema sheria hiyo inakusudia kupunguza matumizi ya fedha kwa taasisi za umma yanayoambatana na taratibu za kumpata mzabuni, pamoja na bei pungufu ya vifaa vinavyouzwa na taasisi yake ikilinganishwa na wafanyabiashara binafsi.

Anasema hiyo ni dhana ya ununuzi wa pamoja inayotekelezwa na taasisi yake inayolenga kuipunguzia gharama za matumizi serikali.

Dhana hiyo imekuwepo katika fani ya ununuzi na ugavi kwa miaka mingi iliyopita.

“Mfumo wa ununuzi wa pamoja katika sekta ya umma umekuwa ukiboreshwa katika vipindi tofauti kabla na baada ya uhuru,” anasema.

Kwa kutambua hilo, serikali ilianzisha taasisi na mifuko mbalimbali kwa ajili ya kusimamia ununuzi na utunzaji wa pamoja wa vifaa na huduma zinazotumiwa na serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Moja ya taasisi hizo ni Bohari Kuu ya Serikali ambapo sasa wakala wake umerithi mfumo wa utendaji wake.

 Mwambega anasema mwaka 1961 kwa kupitia Sheria Na. 21 ya 1961 kifungu cha 18 na 19; Serikali ilianzisha mfuko maalumu wa Bohari  Kuu wa thamani ya sh milioni 24 kwa lengo la kununua, kuhifadhi na kusambaza vifaa mbalimbali kwa matumizi ya Serikali.

Kuhusu vyanzo vya mapato ya wakala anasema wakala unapata fedha za kuendesha shughuli zake kutoka vyanzo mbalimbali kama vile uuzaji wa vifaa kwa taasisi za serikali.

Anasema katika kutekeleza majukumu yake wakala unaongozwa na Mpango Mkakati ambapo kwa sasa unatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2017/2018. Na huo ni mpango mkakati wa tatu tangu kuanzishwa kwa wakala.

Anafafanua kuwa baadhi ya maeneo yanayotiliwa mkazo katika mpango huu ni pamoja na kuimarisha huduma ya ununuzi na ugavi, kuboresha mifumo ya usimamizi wa rasilimali za wakala na kusimamia na kuendeleza rasilimali watu.

Anasema wakala unalenga  kuwa wakala unaoheshimika na sikivu ifikapo mwaka 2025.

Katika kufikia malengo hayo majukumu ya wakala kama yalivyoainishwa chini ya kifungu Na. 21 cha Agizo la Uanzishwaji wa Wakala ni pamoja na kununua, kuhifadhi na kuuza kwa bei za ushindani vifaa vya matumizi ya ofisini, mafuta na vilainisho vya magari na mitambo ya serikali.

Anasema baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na wakala katika utekelezaji wa majukumu yake ni utekelezaji na.

Anafafanua kuwa katika kipindi cha takriban miaka mitano tangu wakala uanzishwe, kumekuwa na ongezeko la wateja na vyanzo vya mapato.

Ongezeko hilo limesababisha kuwepo kwa ongezeko la makusanyo ya mapato kwa kipindi hicho chote.

Mengine anasema ni wastani wa makusanyo ya mapato yatokanayo na mauzo na huduma zitolewazo na wakala yameongezeka kutoka sh 17,668,282,503.00 mwaka 2008/2009 hadi sh 36,790,321,000.00 mwaka 2012/2013 sawa na  ongezeko la asilimia 108,

, wakala umeweza kuhakikisha uwepo wa bidhaa ya mafuta ya kuendeshea magari ya serikali kwa wakati wote katika vituo vyake vyote mikoani isipokuwa mikoa mipya ya Njombe, Geita, Katavi na Simiyu.

“Wakala umeongeza aina ya vifaa maghalani na hivi karibuni imeanza kununua na kuuza aina mbalimbali za wino wa kompyuta,” anasema.

, anasema wakala umeweza kuwapeleka watumishi wake kwenye mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwaongezea weledi na maarifa kwa lengo la kuboresha utendaji wao.

 Mafunzo waliyopata ni pamoja na digrii za uzamili, digrii za kwanza, diploma na cheti, mafunzo ya muda mfupi ndani na nje ya nchi.

“Kumefanyika ziara za mafunzo kwa viongozi katika nchi mbalimbali duniani ili kuweza kujionea jinsi shughuli za ununuzi na utunzaji pamoja na mifumo mbalimbali inavyofanya kazi kwa lengo la kutumika hapa nchini,” anasema na kuongeza kuwa mwaka 2009/2010 wakala ulianzisha utaratibu wa ununuzi wa pamoja wa vifaa na huduma mtambuka kwa kutangaza zabuni moja kwa niaba ya taasisi zote za serikali.

Anabainisha kuwa utaratibu huo unafaida kubwa kwa serikali kwani husaidia katika kupunguza gharama za kuendesha mchakato wa zabuni, hivyo kuwezesha serikali kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ufanisi zaidi.

“Utaratibu huu pia unasaidia kurahisisha upatikanaji wa vifaa na huduma, kupunguza tofauti za bei za vifaa kati ya taasisi za umma pamoja na kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika zabuni za umma hususan kampuni ndogo na za kati ambazo haziwezi kushiriki katika zabuni kubwa,” anasema.

Anafafanua kuwa zaidi ya hayo utaratibu huo husaidia serikali na wazabuni kupata taarifa za ununuzi kutoka sehemu moja.

Tangu kuanzishwa kwake idadi ya wazabuni waliopewa mikataba imekuwa inaongezeka kutoka wazabuni 3,397 mwaka 2009/2010 hadi wazabuni 7,949 mwaka 2012/2013.

Quick Links

Public Notice

Prev Next

STRATEGIC PLAN

19-07-2017

STRATEGIC PLAN FOR THE YEAR 2013/2014 -2017/2018

Read more

NOTIFICATION OF ACCEPTANCE TO SUCCESSFUL TENDERERS…

18-07-2017

18/07/2017   NOTIFICATION OF AWARD TO SUCCESSFUL TENDERERS OF FRAMEWORK AGREEMENTS   RE:   TENDERS FOR COMMON USE ITEMS AND SERVICES USING FRAMEWORK ARRANGEMENTS FOR THE PERIOD OF 2017/2018 Following the Notice of Intention to Award...

Read more

GPSA new ministerial advisory board Inaugurated.

30-01-2017

  The Deputy Minister for Finance and Planning, Honorable Dr. Ashatu Kijaji has directed all Public Institutions to procure their Common Use Items and Services (CUIS) through Government Procurement Services Agency;...

Read more

Government Procurement Notice

14-09-2015

    GENERAL PROCUREMENT NOTICE (GPN) Pursuant to Public Procurement Act, 2011 Section 49(1) and Regulation 69 and 70 of Public Procurement Regulations, 2013. Government Procurement Service Agency is issuing a General...

Read more

PPRA Mobile Tender Alert Service

24-04-2015

The Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) is a regulatory body established under the Public Procurement Act CAP 410 as repealed by the Public Procurement Act No.7 of  2011.The Authority is...

Read more

GPSA kupunguza gharama za ununuzi wa taasisi za um…

14-03-2014

Chanzo: Tanzania Daima , 13 ,March 2014 WAKALA wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wakala za Serikali Na.  30 ya mwaka...

Read more

Public Procurement Regulations 2013

07-03-2014

To download the The Public Procurement Regulations, 2013 click here

Read more

TONER CARTRIDGES! NOW AVAILABLE FOR SALE!

27-02-2014

We have in Stock for sale a number of Toner Cartridges! Rush before the Stock exhausts! To view the list of available Toner Cartridge Click Here

Read more

GPSA Catalog

09-09-2013

To view GPSA stock catalog please click here

Read more

List of Procuring Entities Located In Dar Es Salaa…

04-04-2013

{aridatatables moduleId="167"}

Read more

Visitors Counter

2815553
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
3772
3752
10793
2144661
64767
71885
2815553